Mechi zote za Kombe la Hispania zisitishwa baada ya ajali ya treni Madrid
Test Admin
Mwandishi
Mechi zote 24 za Copa del Rey za Jumatano zimesitishwa baada ya ajali ya treni Toledo iliyoua zaidi ya 30.
| # | Timu | MC | U | Pt |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Man City | 8 | 7 | 21 |
| 2 | Arsenal | 8 | 7 | 21 |
| 3 | Brighton | 8 | 5 | 16 |
| 4 | Liverpool | 8 | 4 | 15 |
| 5 | Chelsea | 8 | 4 | 13 |
| 6 | Brentford | 8 | 2 | 11 |
- Ilichapishwa
Mechi zote 24 za Copa del Rey ya Hispania zilizokuwa zipigwe Jumatano zimesitishwa kama ishara ya heshima baada ya zaidi ya watu 30 kupoteza maisha katika ajali ya treni karibu na Madrid.
Zaidi ya abiria 500 walikuwa wanasafiri kwenye treni hizo zilipogongana na kutoka kwenye njia (derail) huko Toledo.
Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Hispania (RFEF), mamlaka zilisema uamuzi huo umefanyika kwa mshikamano na wahanga.
Timu tano za Ligi Kuu, Levante, Alaves, Valencia, Celta Vigo na Real Betis, zilitarajiwa kucheza mechi za raundi ya kwanza Jumatano.
Mabingwa wakubwa wa Hispania wakiwemo Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid hawatarajiwi kuingia kwenye michuano hiyo hadi raundi ya 32 bora.
Barcelona ilitoa “rambirambi zake za dhati kabisa” kwa wahanga wa ajali hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
“FC Barcelona inatoa rambirambi zake za dhati kabisa kwa wahanga wa ajali mbaya ya reli kati ya Los Yebenes na Urda (Toledo).
“Klabu inapenda kuwasilisha msaada na mshikamano wake kwa familia na marafiki wa wahanga na kuwatakia majeruhi wote wapone haraka.”
Real Madrid nao waliweka ujumbe kwenye tovuti yao wakitoa “msaada kamili” kwa huduma za dharura.
“Real Madrid C. F. inapenda kueleza masikitiko yake makubwa kabisa kuhusu ajali ya kusikitisha ya reli iliyotokea katika mkoa wa Toledo.
“Klabu inatoa rambirambi kwa familia na wapendwa wa waliopoteza maisha, pamoja na kuonyesha upendo na mshikamano kwa majeruhi na wote walioathirika na ajali hii mbaya.
“Real Madrid inapenda kutoa msaada wake kamili kwa huduma za dharura na wote wanaofanya kazi za uokoaji, na inaungana katika majonzi ya kila mmoja aliyeathirika katika nyakati hizi za huzuni kubwa.”
Mechi za Alhamisi zimebaki kama zilivyopangwa, huku RFEF bado haijatoa ratiba mpya ya michuano kwa ajili ya mechi za Jumatano zilizoahirishwa.
Lebo:
Pata habari kwa SMS
Tuma "HABARI" kwenda 22244









